Ilisasishwa mwisho: Machi 2026
Sisi katika Mama Kuchi tunaheshimu sana faragha yako na tumejizatiti kulinda taarifa zako binafsi zinazotambulika.
Tunakusanya jina lako na barua pepe (email) na **kuhifadhi kwa kudumu** ili kutambua akaunti yako na kuhakikisha ufikiaji wako wa mafunzo wakati wote.
Namba ya simu hutumiwa **wakati wa malipo pekee** na haihifadhiwi kwa kudumu kwenye mifumo yetu baada ya muamala kukamilika.
Hatuuzi wala kutoa taarifa zako kwa watu baki bila idhini yako. Taarifa zako za malipo zinapitia mifumo salama ya kifedha iliyoidhinishwa nchini Tanzania.